TAARIFA KWA UMMA : MWALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA KIKAO CHA KUKUSANYA MAONI YA WADAU JUU YA MAOMBI YA NAULI MPYA KWA MELI ZA MV. NJOMBE, MV. MBEYA II NA

Imewekwa: Oct 26, 2022


TAARIFA KWA UMMA

MWALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA KIKAO CHA KUKUSANYA MAONI YA WADAU JUU YA MAOMBI YA NAULI MPYA KWA MELI ZA MV. NJOMBE, MV. MBEYA II NA MV. RUVUMA ZINAZOTOA HUDUMA ZIWA NYASA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limepokea kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) maombi ya viwango vipya vya nauli za abiria na ubebaji wa mizigo kwa safari za meli za Mv. Njombe, Mv. Mbeya II na Mv. Ruvuma zinazofanya safari katika Ziwa Nyasa.

Kwa mujibu wa kifungu cha 29 (2) (b) cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415, Shirika limeandaa mikutano ya wadau wa huduma ya usafiri majini katika Ziwa Nyasa ili kukusanya maoni kuhusu maombi yaliyowasilishwa. Mikutano hiyo itafanyika kama ifuatavyo:

  • Kyela Mjini - tarehe 31 Oktoba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kuanzia saa 4 kamili asubuhi;
  • Manda - tarehe 02 Novemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Water Bay Beach - Manda kuanzia saa 4 kamili asubuhi; na
  • Mbamba Bay - tarehe 04 November, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kapteni John Komba – Mbamba Bay (Nyasa) kuanzia saa 4 kamili asubuhi.

Kwa tangazo hili wadau wote mnaalikwa kushiriki. Wadau wanaweza kutuma maoni kwa njia ya mtandao kupitia barua pepe: tariff@tasac.go.tz au kwa kufika katika ofisi za TASAC – Kyela Mjini au TASAC – Makao Makuu. Maoni pia yanaweza kutumwa kwa njia ya barua kwa anuani ifuatayo: Mkurugenzi Mkuu, TASAC, S.L.P 989, Dar es Salaam. Mwisho wa kupokea maoni ni tarehe 14 Novemba, 2022.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu,

TASAC

25/10/2022