​TAARIFA KWA UMMA MAREKEBISHO YA SHERIA YA UWAKALA WA MELI TANZANIA, SURA YA 415 KUPITIA SHERIA YA FEDHA NA. 5 YA MWAKA 2022

Imewekwa: Jul 08, 2022


TAARIFA KWA UMMA

MAREKEBISHO YA SHERIA YA UWAKALA WA MELI TANZANIA, SURA YA 415 KUPITIA SHERIA YA FEDHA NA. 5 YA MWAKA 2022

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) linapenda kuujulisha umma kuwa, kuanzia tarehe 1 Julai, 2022, litatekeleza majukumu ya kipekee (exclusive mandate) ya ugomboaji na uondoshaji wa shehena aina ya silaha na vilipuzi, makinikia, kemikali zitumikazo kwenye kampuni za uchimbaji madini, nyara za Serikali na wanyama hai kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Uhifadhi wa Wanyama Pori Sura ya 283. Hatua hii inafuatia marekebisho ya Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415 yaliyofanyika kupitia Sheria ya Fedha Na. 5 ya mwaka 2022.

Aidha, kuanzia tarehe 1 Julai, 2022, TASAC haitatekeleza majukumu ya kipekee katika uwakala wa meli (shipping agency), uhakiki wa shehena (ship tallying) na udhibiti wa nyaraka za wakala wa meli (document control for shipping agency).

TASAC inawashukuru wateja wake, wadau wote na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano wao wakati wa kutekeleza majukumu yake.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu

SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA

08 Julai, 2022