Kurugenzi

Huduma za Shirika

Kutoa ushauri na utaalamu kuhusu utawala, usimamizi wa rasilimali watu, mipango, masoko na uhusiano.

Kurugenzi hii ina idara kuu tatu (3) kama ifuatavyo:

 • Usimamizi Rasilimali Watu na Utawala;
 • Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini; na
 • Masoko na Uhusiano.

Kurugenzi ya Biashara Meli

Kusimamia na kutoa utaalamu wa namna ya kufanya biashara ya upokeaji na uondoshaji shehena, uwakala wa meli na huduma za uhakiki wa shehena.

Kurugenzi hii ina idara kuu tatu(3) kama ifuatavyo:

 • Idara ya wakala wa meli,
 • Idara ya uhakiki shehena; na
 • Idara ya upokeaji na uondoshaji shehena.

Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira wa Bahari

Kutoa utaalamu na huduma kuhusu udhibiti na usimamizi wa usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira ya bahari

Kurugenzi hii ina idara kuu (3) kama ifuatavyo:
 • Usajili, Uchunguzi na Ukaguzi wa Meli;
 • Mafunzo na Utoaji vyeti kwa Mabaharia; na
 • Usalama wa uendeshaji meli na Mazingira ya Bahari.

Kurugenzi ya Huduma za Bandari na Usafiri wa Meli

Kutoa ushauri na utaalamu kuhusu udhibiti wa huduma za uchukuzi wa majini (huduma za bandari na usafiri wa meli) ili kuimarisha utekelezaji wa sheria na kuboresha huduma.

Kurugenzi hii ina idara zifuatazo:

 • Idara ya Bandari; na
 • Idara ya Usafiri wa Meli