Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Mbelwa Kairuki akutana na Ujumbe wa Tanzania uliohudhuria Mkutano wa IMO
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Mbelwa Kairuki akutana na Ujumbe wa Tanzania uliohudhuria Mkutano wa IMO
Imewekwa: 23 April, 2024
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Mbelwa Kairuki tarehe 22 Machi, 2024 amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Tanzania uliohudhuria Mkutano wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini (International Maritime Organization -IMO) uliofanyika jijini London.
Katika Mkutano huo, Balozi Kairuki ameuhakikishia Ujumbe huo utayari na wajibu wa Ubalozi kuendelea kuwa kiungo muhimu kati ya taasisi ya IMO na serikali hapa nchini.