Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

BODI YA WAKURUGENZI WA TASAC YAKUTANA NA KATIBU TAWALA MKOA WA RUVUMA

Imewekwa: 05 December, 2024
BODI YA WAKURUGENZI WA TASAC YAKUTANA NA KATIBU TAWALA MKOA WA RUVUMA

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 4 Novemba, 2024 imetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kufanya mazungumzo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Joel Mbewa.

Ujumbe wa Bodi umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, Nah. Mussa Mandia, ambaye amemueleza Kaimu Katibu Tawala kuwa bodi ya TASAC imefika mkoani humo kwa lengo la kufanya ziara ya siku tatu ya kutembelea maeneo ya usafiri majini yanayodhibitiwa na TASAC mkoani humo.

Nah. Mandia amesema kuwa TASAC imejiwekea utaratibu wa kutembelea maeneo wanayoyadhibiti ili kuona kinachoendelea na kupata maoni ya viongozi wa Serikali na wananchi wa maeneo husika.

"Ni utaratibu wa kawaida tuliojiwekea kuembelea maeneo tunayoyadhibiti ili kuona kinachoendelea na kupata maoni ya viongozi wa Serikali na wananchi wa maeneo husika. Hii inatusaidia kuweza kuishauri Serikali na kutoa maelekezo stahiki pale inapohitajika," amesema Nah. Mandia.

Kwa upande wake, Bw. Mbewa ameueleza ugeni huo kuwa mkoa wa Ruvuma upo tayari kushirikiana na TASAC katika kuwahudumia wananchi  wa mkoa huo katika maeneo ya usafiri majini ili kuweza kuchagiza shughuli za maendeleo.

Ziara katika mkoa huo imeanza leo, tarehe 4 Desemba 2024 na inatarajia kukamilika tarehe 6 Desemba 2024 ambapo Bodi itatembelea maeneo ya Mbamba Bay, Liuli, Njambe, Ndumbi na Manda.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo