Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) akiwa katika Mkutano wa waandishi wa habari jijini Mwanza 21 Juni, 2023.

Imewekwa: 23 June, 2023
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) akiwa katika Mkutano wa waandishi wa habari jijini Mwanza 21 Juni, 2023.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali akiwa katika Mkutano wa waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano Katika Ofisi za TASAC jijini Mwanza Uliofanyika Tarehe 21 Juni, 2023.

Akizungumza katika mkutano huo alielezea kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 22 Juni, na kilele chake tarehe 25 Juni. 

Bw. Mlali alieleza kuwa Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanayofanyika jijini Mwanza yataambatana na Maonesho ya Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na Sekta ya Usafiri Majini, Ufanyaji usafi katika Mialo na maeneo mengine, utoaji elimu kwa wadau mbalimbali na wanafunzi wa vyuo ili kuleta kwa Vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika Sekta ya Usafiri Majini.

Aidha, Bw. Mlali ametoa rai kwa Wananchi wa Jijini Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria kwa wingi ili kupata Elimu kuhusu mabaharia na Sekta ya Maji kwa ujumla.

Kauli mbiu ya Maadhimisho haya mwaka huu ni "Miaka 50 ya MARPOL Uwajibikaji wetu Unaendelea."

Mrejesho, Malalamiko au Wazo