Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Katika kuelekea kilele cha Siku ya Bahari Duniani tarehe 28  ya maji wametembelea shule za sekondari, soko pamoja na madiko (mialo), visiwani Pemba - Zanzibar,  tarehe 26 Septemba, 2023.

Imewekwa: 07 October, 2023
Katika kuelekea kilele cha Siku ya Bahari Duniani tarehe 28  ya maji wametembelea shule za sekondari, soko pamoja na madiko (mialo), visiwani Pemba - Zanzibar,  tarehe 26 Septemba, 2023.

Katika kuelekea kilele cha Siku ya Bahari Duniani tarehe 28  ya maji wametembelea shule za sekondari, soko pamoja na madiko (mialo), visiwani Pemba - Zanzibar,
 tarehe 26 Septemba, 2023.
Lengo la kutembelea maeneo hayo ni kutoa elimu kuhusu fursa zilizopo katika sekta usafiri majini, masuala ya usalama wa abiria na vyombo ambapo jumla ya majaketi okozi 200 (life jackets) yalitolewa kwa kamati za uvuvi za Sheia katika madiko (fukwe).

Shule za sekondari ambazo zilipewa elimu Chokocho, Fundo, Fidarkasto, Pindua, Mkanyageni na Micheweni. 

Kwa upande wa madiko (mialo) yaliyopata fursa ya kupata elimu hiyo pamoja na majaketi ni Diko la Makongwe, Fundo, Kojani, kisiwa Panza, lakini pia soko la Tumbe.

Wananchi na wanafunzi kwa ujumla wamewashukuru wadau hao kwa kuweza kuwapatia elimu ambayo wengi wao hawakuwa wanaifahamu.

Wadau walioshiriki katika utoaji elimu  hiyo ni Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ), Wizara ya Uchukuzi (SMT), Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Shirika la Uwaka wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC), Chuo cha Mabaharia Dar es salaam (DMI), Chama cha Mabaharia Zanzibar (ZASU), Chama cha Mabaharia Tanzania (TASU), Polisi wanamaji, Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Shirika la Meli Zanzibar (SHIPCO), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Zanzibar (KZU), na Taasisi ya Wanawake walioko katika sekta ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika (WOMESA)

Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani kwa mwaka 2023 yenye Kauli mbiu "Miaka 50 ya MARPOL, uwajibikaji wetu Unaendelea" Kitaifa yanafanyika visiwani Pemba-Zanzibar katika viwanja vya Gombani Nje, yalifunguliwa rasmi tarehe 25 Septemba, 2023 na yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 28 Septemba, 2023.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo