Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Maonesho ya Kongamano la Wiki ya Pili ya Ufuatiliaji (U&T) AICC - Arusha

Imewekwa: 07 October, 2023
Maonesho ya Kongamano la Wiki ya Pili ya Ufuatiliaji (U&T)  AICC - Arusha

MAONESHO YA KONGAMANO LA WIKI YA PILI YA UFUATILIAJI (U&T) 12-15 SEPTEMBA 2023 ARUSHA - AICC

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni kati ya Taasisi za Kiserikali zinazoshiriki maonesho yanayoendelea katika Kongamano la Wiki ya Pili ya Ufuatiliaji (U&T).
Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya AICC jijini Arusha yalianza tarehe 12 Septemba na kilele chake ni tarehe 15 Septemba, 2023. 

TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu kazi  na majukumu inayoyatekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.

Wadau wote mnaalikwa kutembelea banda la TASAC katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo