Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mhe. Atupele Mwakibete (MB) atembelea banda la TASAC katika Maonesho ya Nanenane, Mkoani Mbeya.

Imewekwa: 02 August, 2023
Mhe. Atupele Mwakibete (MB) atembelea banda la TASAC katika Maonesho ya Nanenane, Mkoani Mbeya.

Mhe. Atupele Mwakibete ( MB), Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi, leo ametembelea banda la TASAC ikiwa ni moja ya Taasisi za Kiserikali chini ya Sekta ya Uchukuzi zinazoshiriki Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima yanayotambulika kama NaneNane.

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Mwakangale Mkoani Mbeya yameanza tarehe 1 Agosti na kilele chake ni tarehe 8 Agosti, 2023. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni:- “ Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo ya Chakula na Usalama wa Chakula ”.

TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi  na majukumu yanayotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri ameipongeza TASAC kwa Udhibiti wa Usafiri Majini na kulisihi Shirika hilo kutumia taarifa za Sensa ya Vyombo Vidogo kuongeza mapato kwa Taifa.

TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea banda la TASAC lililo katika eneo la Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo