Mkurugenzi Mkuu TASAC awasilisha mada katika Mkutano wa 16 wa wadau Sekta ya Uchukuzi.
Mkurugenzi Mkuu TASAC awasilisha mada katika Mkutano wa 16 wa wadau Sekta ya Uchukuzi.
Imewekwa: 16 January, 2024
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Malick Salum amewasilisha mada katika Mkutano wa 16 wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa Arusha (Arusha International Conference Centre- AICC) leo tarehe 07 Disemba, 2023.
Katika wasilisho hilo Bw. Salum ameelezea majukumu, fursa, na mafanikio ya Shirika hilo linalofanya kazi zake katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji.