Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amekutana na wasafirishaji wa shehena kwa malori na wateja/mawakala wao.

Imewekwa: 28 April, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amekutana na wasafirishaji wa shehena kwa malori na wateja/mawakala wao.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala Wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, amekutana na wasafirishaji wa shehena kwa malori na wateja/mawakala wao ili kujadili muda wa bure wa makasha na tozo za ucheleweshaji makasha hususani yanayokwenda DRC Congo na kurejeshwa.


Kikao hiki cha siku moja kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii, jijini Dar es Salaam kilihudhuliwa na wadau mbalimbali wa usafirishaji majini.
Katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu aliwaambia wadau hao kuwa Serikali yetu imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na changamoto zinazochelewesha urejeshaji wa makasha kwa wakati.

Aidha, aliongeza kuwa kumekuwa na mawasiliano baina ya nchi ya Tanzania na nchi jirani ili kuwezesha utatuzi wa changamoto ambazo ziko nje ya mipaka yetu.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo