Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amewatunuku vyeti wahitimu wa Kozi ya muda mfupi ya Uhakiki Shehena kutoka nchini Kenya.

Imewekwa: 28 April, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amewatunuku vyeti wahitimu wa Kozi ya muda mfupi ya Uhakiki Shehena kutoka nchini Kenya.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amewatunuku vyeti wahitimu wa Kozi ya muda mfupi ya Uhakiki Shehena (Cargo Tallying) kutoka Kenya katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es salaam tarehe 06 April, 2023.

Akizungumza katika Mahafali hayo Bw. Mkeyenge amesema kozi hiyo inaenda kuwafanya wahitimu hao kuwa wafanyakazi wazuri katika maeneo ya uingizaji na uondoshwaji wa shehena lakini pia katika maeneo ambayo ufungwaji wa shehena unafanyika katika maeneo ya bandari.

Aidha aliongeza kuwa madhumuni ya Kozi hiyo ni kuwajengea vijana uwezo na ujuzi wa kuwa wahakiki wazuri wa shehena zinazotoka nje na kuingia ndani ya nchi za Afrika Mashariki pamoja na zinazotoka nchini kwenda nchi nyingine kwa kutumia vyombo vya usafiri majini.

Pia Bw. Mkeyenge amesema sekta ya usafiri majini imepiga hatua hivyo amewasihi vijana kuchangamkia fursa kwa kusoma Kozi zinazohusu sekta hiyo.

" Sekta hii imepiga hatua katika ukanda wa Afrika Mashariki hivyo ni muhimu kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uwezo madhubuti, hivyo nawasihi vijana kuchangamkia fursa ya kusomea Kozi zinazohusu sekta hii ili kuendelea kuzalisha wataalamu wengi zaidi". Alisema Mkeyenge.

Jumla ya wanafunzi 22 kutoka Chuo cha Kenya Coast National Polytechnic (KCNP) wamehitimu Kozi hiyo ya mwezi mmoja katika Chuo cha Usafirishaji (NIT).
 

Mrejesho, Malalamiko au Wazo