Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC akutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Afrika wa Kampuni ya “China Classification Society” (CCS) kujadiliana juu ya sekta ya usafiri majini

Imewekwa: 20 July, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC akutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Afrika wa Kampuni ya “China Classification Society” (CCS)  kujadiliana  juu ya sekta ya usafiri majini

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Afrika wa Kampuni ya “China Classification Society” (CCS) Bw. Jacob Chan na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya usafiri majini.  Ujio huu wa Bwana Jacob ni pamoja na kuitambulisha kampuni hiyo ya CCS kwa TASAC kama Mawakala wa kusimamia usalama na ubora wa ujenzi wa vyombo vya usafiri majini na katika uendeshaji wa meli zilizosajiliwa kimataifa. 

Kampuni ya CCS ni moja kati ya  Taasisi zinazotambulika (Recognized Organizations, ROs) ambayo inashughulika na masuala ya ukaguzi wa meli na iwapo TASAC ikikamilisha mapitio ya kanuni ya ROs na kuanza kutumika itaweza kuikasimu Kampuni hiyo madaraka ya kukagua na kutoa baadhi ya vyeti kwa meli za kimataifa ambazo zimesajiliwa na Tanzania kupitia TASAC. 

CCS ni mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Viwango vya Ujenzi wa Meli (International Association of Classification Society, IACS) ambayo inatambulika na Shirika la Bahari Duniani kama washauri wakuu wa masuala ya ukaguzi wa usalama wa vyombo vya usafiri majini na utoaji wa vyeti vya ubora.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo