Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, amefanya mazungumzo na wawakilishi wa Wizara ya Uvuvi na Rasilimali za Bahari (MFMR) kutoka Namibia

Imewekwa: 13 October, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, amefanya mazungumzo na wawakilishi wa Wizara ya Uvuvi na Rasilimali za Bahari (MFMR) kutoka Namibia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Wizara ya Uvuvi na Rasilimali za Bahari (MFMR) kutoka Jamhuri ya Namibia walipotembelea ofisi za TASAC wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kiufundi Bw. Steven Ambabi na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya usafiri majini, hususani katika mafunzo na utoaji vyeti kwa Mabaharia Leo tarehe 12 Oktoba, 2023 jijini Dar es Salaam.

Lengo la ujio huo ni kujenga mahusiano ya kirafiki kwa TASAC na Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) na kuelezea namna ya vigezo vya kujiunga katika kozi za ubaharia  kwa mabaharia kutoka Namibia kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Aidha, Bw. Mkeyenge amewakaribisha na kuwaeleza kuwa Tanzania ni nchi ambayo imepiga hatua katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji na ni nchi mwanachama wa  Shirika la Bahari Duniani (IMO) ambayo imeridhia Mikataba mbalimbali ya IMO, ikiwepo Mkataba wa Kimataifa wa Mafunzo,  utoaji  vyeti na ufanyaji kazi kwa Mabaharia STCW 78.

Ziara hiyo ya siku mbili itajumuisha kutembelea Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) ambako watapata fursa ya kujifunza  na kuona shughuli zinazofanywa na chuo hicho.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo