Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amewapongeza wahitimu wa shule ya Kiislamu ya Msingi na Awali kwa kuwataka kutumia elimu waliyopata kuleta mabadiliko kwa jamii.

Imewekwa: 30 October, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amewapongeza wahitimu wa shule ya Kiislamu ya Msingi na Awali kwa kuwataka kutumia elimu waliyopata kuleta mabadiliko kwa jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amewapongeza wahitimu wa shule ya Kiislamu ya Msingi na Awali kwa kuwataka kutumia elimu waliyopata kuleta mabadiliko kwa jamii katika Mahafali yaliyofanyika Mikocheni tarehe 21 Oktoba, 2023.

Akizungumza katika mahafali hayo 
Bw. Mkeyenge amesema  kuwa “Hii ni siku yenu ya kujivunia kazi ngumu mliyoifanya kwa miaka hii yote, hongereni sana. Ninaamini kuwa elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo na mabadiliko katika jamii. Wanafunzi mnayo nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu. Ni matumaini yangu kuwa mtatumia elimu mliyoipata hapa kuwa raia wema na kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu."

Aidha, amefurahishwa sana na kutoa pongezi za dhati kwa uongozi wa shule hiyo kwa kumchagua kuwa Mgeni Rasmi wa mahafali hayo, alipongeza maendeleo mazuri ya taaluma ya shule hiyo kwa kuridhishwa na matokeo ya Wilaya na Mkoa na Pia amaefurahishwa na michezo mbalimbali iliyooneshwa na wanafunzi wakati wa mahafali hayo na kupongeza mipango ya kupambana kuongeza eneo la shule kwa ajili ya kuendeleza masomo ya Sekondari kwa wanafunzi wanaomaliza shuleni hapo ili kutopoteza maadili waliyofundishwa. 

Pia Bw. Mkeyenge alitoa pongezi kwa walimu, wazazi na walezi kwa jukumu kubwa wanalolifanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo