Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile  ameipongeza TASAC kwa usimamizi na udhibiti makini na utoaji wa haraka wa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa

Imewekwa: 07 October, 2023
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile  ameipongeza TASAC kwa usimamizi na udhibiti makini  na utoaji wa haraka wa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile  amelipongeza Shirika  la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa usimamizi na udhibiti makini wa vyombo vinavyotumia usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa haraka wa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau mbalimbali hivyo kuwahakikishia usalama wao.

Akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya TASAC, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kahenzile wakati  wa ziara yake ya kujifunza, kujitambulisha na kukagua ofisi za Shirika hilo pamoja na  kutembelea miradi mbalimbali ya udhibiti na usimamizi wa vyombo vya usafiri Nchini kikiwemo kituo cha Kuratibu shughuli za Utafutaji na Uokoaji Majini (MRCC) vyote vilivyopo Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Septemba, 2023.

Mhe. Kihenzile ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miradi ya kimkakati nchini ikiwemo upanuzi wa bandari, ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo pia kuendelea kutafuta wadau binafsi wa kushirikiana nao kuziendesha hali itakayosababisha ujio wa meli zaidi Nchini na kuwahakikishia Maji ya Tanzania yako salama.

“Nimepata fursa pia ya kutembelea kituo cha kuratibu Shughuli za utafutaji na uokoaji majini, vituo hivi vinajengwa nchi nzima kwenye bahari zetu na maziwa hivyo niwahakikishie wadau na watumiaji wa vyombo vya usafiri majini, maji ya Tanzania yako salama, bahari zetu na maziwa yetu ni salama katika usafirishaji kwa njia ya maji tumieni fursa hii kuwekeza zaidi  kwenye njia hii ya usafirishaji kwani ni rahisi, salama na ya gharama nafuu". Amesisitiza Kihenzile.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali alimshukuru Naibu Waziri kwa kuchukua hatua ya kutembelea Taasisi zote zilizo chini ya Wizara na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Shirika ikiwemo uanzishwaji wake, mafanikio, miradi mbalimbali, changamoto pamoja na Mikakati ya kukabiliana nazo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo