Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Serikali ina malengo mahsusi na Sekta ya Usafiri wa Majini.

Imewekwa: 21 November, 2023
Serikali ina malengo mahsusi na Sekta ya Usafiri wa Majini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Mohamed Malick Salum amesema kuwa Serikali ina malengo mahususi katika sekta usafiri majini katika kukuza uchumi wa taifa letu Tanzania. Jukumu la utekelezaji wa malengo hayo linafanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ikiwa chini ya uongozi wa Wizara ya Uchukuzi.

Kutokana na umuhimu TASAC kwa ajili ya kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa na kuinua uchumi wa Taifa Bw. Mohamed Malick Salum amesema, "Naomba ushirikiano wenu menejimenti na wafanyakazi pamoja ili kukamilisha utekelezaji wa majukumu haya tuliominiwa na Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan."

Aidha, Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge naye alisema kuwa anashukuru menejimenti ya TASAC kwa kumpa ushirikiano kwa chote cha uongozi wake na kusema amempa Mkurugenzi Mkuu mpya nyezo za kufanyia kazi. 

"Nimempa dira ya TASAC na mpango mkakati ili aendeleze kuongoza hili Shirika, maana  huyu ni mzoefu na amesomea mambo ya sekta ya usafiri majini, sisi wote ni serikali moja tuendelee kushirikiana katika maeneo tutakayoona tunahitajiana ili kujenga uchumi wa taifa hili.

Bw. Mohamed aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu tangu  tarehe 14 Novemba, 2023  baada Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa.

Makabidhiano ya Ofisi yamefanyika katika ofisi ya  Mkurugenzi Mkuu wa TASAC katika jengo la PSSSF Tower Garden Avenue leo Ijumaa tarehe 17 Novemba, 2023.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo