Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Tanzania kutambuliana vyeti vya Mabaharia na Barbados

Imewekwa: 07 October, 2023
Tanzania kutambuliana vyeti vya Mabaharia na Barbados

Kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini Hati ya Makubaliano (MOU) ya kutambuliana vyeti vya mabaharia na nchi ya Barbados leo tarehe 03 Oktoba, 2023.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC na Msajili wa Mabaharia na Meli nchini Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amesema hadi sasa Tanzania imeanzisha mawasiliano na majadiliano na Nchi 34 kwa ajili ya kuingia katika makubaliano ya kutambuliana vyeti vya Mabaharia (Memoranda of Understanding – MoUs) ili kufungua fursa ya ajira kwa mabaharia wetu, lakini pia kuondoa usumbufu wa kushushwa kwa mabaharia wa kitanzania katika meli mbalimbali ambazo zimesajiliwa na nchi ambazo Tanzania haina mkataba nazo.

“Barbados ni moja ya nchi ambazo tulikuwa tumeanzisha mazungumzo  kuhusu kutambuliana vyeti na tunashukuru leo hii tumefanikiwa kusaini Hati ya Makubaliano ya kutambuliana vyeti vya mabaharia, hivyo basi, ni dhahiri kuwa sisi tunatambua mabaharia wa Barbados na wao wanatambua mabaharia wetu”, amesema Bw. Mkeyenge.

Nchi nyingine ambazo Tanzania imeshaanzisha mawasiliano na majadiliano  ni pamoja na Bahamas, Algeria, Korea ya Kusini, China, Comoros, Cyprus, Misri, Ufaransa, Ghana, India, Iran, Kenya, Liberia, Malta, Marshall Islands, Mongolia, Oman, Palau, Panama, Peru, Qatar, Saudi Arabia, Singapore, Africa Kusini, Sycheles, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu, Vanuatu, Vietnam na nchi za Umoja wa Ulaya.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo