Habari

Imewekwa: 24/07/2021

​TASAC NA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUFANYA SENSA YA VYOMBO VYA USAFIRI WA NJIA YA MAJI TANZANIA.

​TASAC NA OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUFANYA SENSA YA VYOMBO VYA USAFIRI WA NJIA YA MAJI TANZANIA.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la uwakala wa meli nchini (TASAC) Kaimu Mkeyenge (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya takwimu, Dkt. Albina Chuwa wakibadilishana hati ya utilianaji saini wa makubaliano ya kushirikiana na ofisi ya Taifa ya takwimu katika kufanya sensa ya kwanza ya aina yake kwa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji Tanzania Bara. Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 18 Juni 2021 jijini Dodoma.

Katika zoezi hilo, TASAC itatoa utaalamu wa usafiri kwa njia ya maji, wakati Ofisi ya Takwimu ya Taifa itatoa utaalamu wa kufanya sensa.

Faida zitakazopatikana kutokana na sensa hiyo ni pamoja na kuandaa kanzidata ya vyombo vya usafiri nchini ambayo itatumika kuboresha sera, mipango na usimamizi wa sheria na kanunizinazohusu usafiri majini na kusaidia katika ufuatiliaji wa matokeo ya utekelezaji wa sera au mipango mbalimbali. Zoezi hili pia litasaidia katika ukusanyaji wa takwimu na kuwezesha ufanyaji wa tafiti mbalimbali, kufanya maamuzi ya uwekezaji na biashara kuhusu vyombo vya usafiri majini na usafiri kwa njia ya maji kwa ujumla.