Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC imekutana na kufanya mazungumzo na  Afisa Uhusiano wa masuala ya Ulinzi wa Usafiri kwa Njia ya Maji wa  Uingereza, Bi. Patricia Davis tarehe 19 Oktoba, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Imewekwa: 27 October, 2023
TASAC imekutana na kufanya mazungumzo na  Afisa Uhusiano wa masuala ya Ulinzi wa Usafiri kwa Njia ya Maji wa  Uingereza, Bi. Patricia Davis  tarehe 19 Oktoba, 2023  Jijini Dar es Salaam.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekutana na kufanya mazungumzo na  Afisa Uhusiano wa masuala ya Ulinzi wa Usafiri kwa Njia ya Maji wa  Uingereza, Bi. Patricia Davis mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya Leo tarehe 19 Oktoba, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa TASAC Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bi. Leticia Mtaki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira ya Usafiri kwa Njia ya Maji  TASAC amewakaribisha na kuwaeleza kuwa Tanzania ni nchi ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji na ni nchi mwanachama wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) ambayo imeridhia Mikataba mbalimbali ya IMO, ikiwepo Kanuni ya ISPS code.

Bi. Mtaki ameelezea furaha yake kuhusu mpango wa mafunzo hayo ambao utaleta tija kwa Shirika na kwamba ataendeleza ushirikiano ambao tayari ulishajengwa baina ya Uingereza na Tanzania kupitia ofisi hiyo ya Nairobi ambayo inajihusisha na mambo ya usalama wa usafiri wa maji katika eneo la chini ya Jangwa la Sahara

Kwa upande wa Afisa Uhusiano wa Masuala ya Ulinzi wa Usafiri kwa Njia ya Maji Uingereza Bi. Patricia Davis ameeleza kuwa lengo la ujio wao ni kutaka kutambuana na kufahamiana na Mkurugenzi mpya wa Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira TASAC lakini pia kuelezea juu ya mipango ya ofisi yake katika ushirikiano na TASAC ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo yanayohusu Usalama wa Usafiri kwa Njia ya Maji kama sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya Kimataifa kuhusu Usimamizi wa masuala ya Usalama wa Meli na Bandari (ISPS Code). 

Bi. Patricia ameongeza kuwa mipango waliyonayo ni kuendeleza mafunzo kwa maafisa wa TASAC, maafisa wa Bandari na wadau wanaohusika na masuala ya usalama wa Bandari pamoja na meli. 
 
Aidha, amesema kuwa suala la Usalama wa Usafirishaji kwa njia ya maji ni suala linalohitaji ushirikiano wa kimataifa na kwamba TASAC ipo katika harakati za kukamilisha maandalizi ya  Sera ya Taifa ya Ulinzi na Usalama wa Usafiri kwa njia ya maji (National Strategy for Maritime Security) ambayo itaiongoza Tanzania kwenye masuala ya usalama wa Usafirishaji kwa njia ya maji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo