Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC na Wizara ya Uchukuzi wakutana na wadau katika Mkutano wa Wadau wa Kupokea Maoni Kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia  Mkataba wa Afrika wa Usafiri Majini

Imewekwa: 23 April, 2024
TASAC na Wizara ya Uchukuzi wakutana na wadau katika Mkutano wa Wadau wa Kupokea Maoni Kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia  Mkataba wa Afrika wa Usafiri Majini

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi wamekutana na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na binafsi katika Mkutano wa Wadau wa Kupokea Maoni Kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia  Mkataba wa Afrika wa Usafiri Majini uliofanyiwa marejeo mwaka 2010 (Revised African Maritime Transport Charter, 2010). 

Mwenyekiti wa Mkutano huo alikuwa ni Bw. Maseke Mabiki, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Uchukuzi (DPP)  akiwa na mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Wakili. Judith Kakongwe, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria (DLS).

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere ( JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 26 Machi, 2024.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo