Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yafanya semina ya kutoa elimu kwa kamati ya kudumu ya sheria ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani

Imewekwa: 12 September, 2023
TASAC yafanya semina ya kutoa elimu kwa kamati ya kudumu ya sheria ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanya semina ya kutoa elimu kwa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika katika ukumbi wa  Bunge leo tarehe 3 Septemba, 2023 Jijini Dodoma.

Semina hiyo ililenga kutoa uelewa kwa Kamati hiyo kuhusu majukumu miradi na mapato ,  Mpango Mkakati , mafanikio, fursa pamoja na changamoto zinazoikabili TASAC na Sekta ya Usafiri kwa njia ya Maji nchini. 

Katika Semina hiyo, wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti Mhe. Simai Hassan Sadik (MB), wameishukuru Serikali kupitia TASAC kwa kutoa semina hiyo ambayo imejibu na kuleta uelewa wa masuala mbalimbali ambayo yatawapa urahisi Kamati hiyo katika utendaji na kuishauri Serikali kuhusu Sekta ya Usafiri kwa njia ya Maji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo