Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yaibuka mshindi wa pili katika kufikia malengo kulingana na majukumu inayotekeleza.

Imewekwa: 16 January, 2024
TASAC yaibuka mshindi wa pili katika kufikia malengo kulingana na majukumu inayotekeleza.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imepokea tuzo ya mshindi wa pili kutokana na kufikia malengo kulingana na majukumu yanayotekelezwa na Shirika. Tuzo hiyo imetolewa katika Mkutano wa 16 wa Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi (Joint Transport Sector Review Meeting- JSTR) leo tarehe 06 Desemba, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.

Aidha, tuzo hiyo imekabidhiwa na Mhe. Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Mohamed Malick Salum.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo