Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yashiriki Maonesho ya 10 ya Biashara Mkoani Tanga (Tanga Trade Fair) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwahako jijini Tanga kuanzia tarehe 28 Mei hadi 06 Juni, 2023

Imewekwa: 08 June, 2023
TASAC yashiriki Maonesho ya 10 ya Biashara Mkoani Tanga (Tanga Trade Fair) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwahako jijini Tanga kuanzia tarehe 28 Mei hadi 06 Juni, 2023

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika Maonesho ya 10 ya Biashara Mkoani Tanga “Tanga Trade Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako. Maonesho hayo yalianza tarehe 28 Mei, 2023 na kufunguliwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Conrad Milinga na kumalizika tarehe 6 Juni, 2023 yaliyofungwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Mh. Waziri Waziri Kindamba. 
Kauli mbiu ya maonesho hayo kwa mwaka huu ni "Kilimo, Viwanda, Utalii, Madini ndio Maendeleo ya Kiuchumi”

Lengo la TASAC kushiriki maonesho haya ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu inayotekeleza. 
Mojawapo
ya majukumu hayo ni kudhibiti Usalama, Ulinzi wa Vyombo vya Usafiri Majini na Utunzaji wa Mazingira ambayo vyombo hivyo hufanya shughuli zake.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo