Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Wakufunzi Mabaharia wanolewa

Imewekwa: 22 March, 2023
Wakufunzi Mabaharia wanolewa

Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mha. Michael Magesa amefungua mafunzo yaliyotolewa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) kwa Mabaharia wakufunzi ili kuzalisha wanafunzi wenye sifa kimataifa. Katika ufunguzi huo Mha. Magesa amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa ajili ya kuzalisha wataalamu waliothibitishwa kimataifa yanayozingatia viwango kutokana na utendaji wake kuhusu nchi mbalimbali Duniani.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Abdi Mkeyenge alisema lengo la mafunzo hayo ni kukuza kiwango cha elimu kwa mabaharia wa Tanzania ili kukuza fursa za ajira zao Duniani. Alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa siku tano kwa washiriki 35 wakiwemo wakufunzi watumishi wa TASAC na wajumbe wa bodi ya usahihishaji wa mitihani ya bahari.

Aidha, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo, alisema washiriki wa mafunzo hayo watajifunza namna ya kuandaa masomo kwa kuzingatia miongozo ya elimu na mafunzo kwa mabaharia wanaosimamiwa na DMI.

Alisema baada ya mafunzo washiriki watapewa vyeti na IMO itakuwa inafanya ukaguzi baada ya miaka mitano ili kuona kama Chuo kinatoa mafunzo kwa kuzingatia viwango vya kimataifa. Miongozo ya kimataifa inatoa maelekezo ya sifa za wanaofundisha mabaharia namna ya kuaanda somo, ufundishaji na namna ya katunga mitihani. Tuliomba mafunzo haya ili kuwa kuendelea kuwa katika viwango vya kimataifa” alisema.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo