Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Wananchi wakipata elimu walipotembelea banda la TASAC katika maonesho ya OSHA katika viwanja vya Tumbaku, Mkoani Morogoro.

Imewekwa: 28 April, 2023
Wananchi wakipata elimu walipotembelea banda la TASAC katika maonesho ya OSHA katika viwanja vya Tumbaku, Mkoani Morogoro.

Wananchi wakipata elimu walipotembelea banda la TASAC ikiwa ni moja ya Taasisi za Serikali zinazoshiriki maonesho ya OSHA yanayoendelea katika viwanja vya Tumbaku, Mkoani Morogoro.

TASAC inashiriki maonesho hayo yaliyoanza tarehe 26 Aprili 2023 na yatamalizika tarehe 1 Mei, 2023.

Lengo la maonesho haya ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi. Maonyesho haya yanatumika pia kutoa elimu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Mazingira salama na afya ni kanuni na Haki ya msingi mahala pa kazi".
 

Mrejesho, Malalamiko au Wazo