Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yashiriki Mkutano wa 16 wa tathmini ya utendaji wa Sekta ya Uchukuzi.

Imewekwa: 16 January, 2024
TASAC yashiriki Mkutano wa 16 wa tathmini ya utendaji wa Sekta ya Uchukuzi.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki katika Mkutano wa 16 wa Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi (Joint Transport Sector Review Meeting- JSTR) katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Center (AICC) jijini Arusha.

Mkutano huo unaofanyika kwa siku nne (tarehe 05 hadi 8 Desemba, 2023) umeambatana na Maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi za Sekta ya Uchukuzi.

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Mhe. Prof. Godius Kahyarara amefungua maonesho hayo ambapo pia alipata fursa ya kutembelea banda la TASAC na kupata maelezo ya kina kuhusu historia, majukumu, fursa na mafanikio ya Shirika hilo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria (DLS), Wakili. Judith Kakongwe.

TASAC inashiriki Maonesho hayo ikiwa na lengo la kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na mabadiliko yake.

TASAC inawaalika wadau wote wa mkoa wa Arusha na viunga vyake kutembelea katika banda hilo kupata elimu zaidi kuhusu sekta ya usafiri kwa njia ya maji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo