Habari

Imewekwa: 16/09/2019

WARSHA YA WADAU KWENYE MPANGO WA TAIFA WA KUJIANDAA NA KUPAMBANA NA UMWAGIKAJI WA MAFUTA KWENYE BAHARI NA MAZIWA

WARSHA YA WADAU KWENYE MPANGO WA TAIFA WA KUJIANDAA NA KUPAMBANA NA UMWAGIKAJI WA MAFUTA KWENYE BAHARI NA MAZIWA

TASAC ilifanikiwa kufanya Warsha wa Wadau kwenye Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kupambana na Umwagikaji wa Mafuta kwenye Bahari na Maziwa (National Marine Oil Spill Contigency Plan- NMOSRCP .

Mafunzo haya yalifanyika katika ukumbi wa Bandari kuanzia tarehe 10-12 Septemba 2019.


TASAC imekuwa na jukumu la kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na umwagikaji wa mafuta kutokana na Umwagikaji wa Mafuta kwenye Bahari na Maziwa. Shirika kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali ilandaa Mpango huu sambamba na matakwa ya Mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania iliridhia.

Lengo la Warsha ni kufundisha wadau kujiandaa kwa kupambana na Umwagikaji wa mafuta baharini au ziwani pindi itakapotokea hali hii.

Aidha warsha hii imefunguliwa na Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu pamoja na watendaji wa TASAC. Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa nadharia kupitia uwasilishaji wa mada mbalimbali na kwa njia ya vitendo.