Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Mkurugenzi Mkuu TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge akieleza Majukumu na Mafanikio ya TASAC katika Miaka miwili ya Mh. Dkt Samia.

Imewekwa: 22 March, 2023
Mkurugenzi Mkuu TASAC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge akieleza Majukumu na Mafanikio ya TASAC katika Miaka miwili ya Mh. Dkt Samia.

Ndani ya miaka miwili TASAC imeimarisha usimamizi wa ulinzi na usalama wa usafiri majini na kuzuia uchafuzi wa mazingira ya majini utokanao na shughuli za usafiri majini pamoja na kuainisha matokeo yake kwenye mchango wa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.

TASAC ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 23 Februari, 2018.

TASAC imerithi majukumu haya ya udhibiti wa huduma za usafiri majini, usimamizi wa ulinzi na usalama wa usafiri majini na uzuiaji wa uchafuzi wa mazingira utokanao na shughuli za usafiri majini kutoka kwa iliyokuwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

MAJUKUMU YA TASAC

▫️Kutoa huduma za Uwakala wa Forodha kwa Baadhi  ya  Shehena,

Shehena zinazohudumiwa na TASAC ni pamoja na: silaha na vilipuzi, makinikia, kemikali zitumikazo kwenye kampuni za uchimbaji madini, nyara za Serikali na wanyama hai.

▫️Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Usafiri Majini na Kuzuia  Uchafuzi wa Mazingira utokanao na shughuli za usafiri majini (Maritime Administration).

▫️ Kufanya ukaguzi wa meli zilizosajiliwa nchini na meli za nje zinazoingia na kutoka katika bandari za Tanzania Bara, kudhibiti vivuko vyote, kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji majini.

▫️Kudhibiti utunzaji wa mazingira dhidi ya uchafuzi utokanao na shughuli za meli na kutoa taarifa na uelewa kwa umma kuhusu masuala ya ulinzi, usalama na mazingira majini.

▫️Kudhibiti Watoa Huduma za Usafiri Majini Tanzania Bara.

▫️Kutoa, kuhuisha au kufuta leseni za watoa huduma, kusimamia utekelezaji wa viwango vya huduma zinazodhibitiwa, kuweka na kusimamia masharti ya utoaji wa huduma zinazodhibitiwa, kudhibiti tozo na kuhakikisha ushindani miongoni mwa watoa huduma, kufuatilia utendaji wa watoa huduma, kuwezesha utatuzi wa malalamiko katika sekta inayodhibitiwa, kusimamia mienendo ya watoa huduma katika sekta; naKutoa taarifa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu majukumu ya Shirika.

MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA TASAC KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

Mradi wa Uundaji wa Kanzidata ya Vyombo Vidogo vya Usafiri Majini Tanzania Bara.

Mradi wa Kimataifa wa Mawasiliano na Uchukuzi katika Ziwa Victoria (Multi-National Lake Victoria Maritime Communication and Transport – MLVMCT) Ili kukuza uwekezaji katika shughuli za usafiri majini na uvuvi.

- Lengo la mradi huu ni kujenga vituo vinne vya uokozi katika maeneo ya Kanyala – Sengerema, Musoma - Mara, Nansio - Ukerewe na Ilemela – Mwanza  ambavyo vitasaidia katika kushughulikia changamoto za usafiri kwa njia maji na katika uokozi majini.

- Kuimarisha usalama wa vyombo vya usafiri kwa njia maji na kuongeza fursa za kiuchumi kwa jamii zinazoishi kandokando ya Ziwa Victoria (Tanzania na Uganda umepangwa kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 59.23) na unategemewa kukamilika Desemba, 2024.

Uendelezaji na Uimarishaji wa Miundombinu ya Mifumo ya TEHAMA katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini.

Kuunda nyenzo za udhibiti wa huduma za usafiri kwa njia ya maji ikiwa ni pamoja na kanuni na miongozo mbalimbali ambapo jumla ya kanuni mpya 11 zimeshaandaliwa na kuanza kutumika.

Kuwashirikisha wadau katika maamuzi ya kiudhibiti na masuala mengine yanayowahusu ili kuimarisha mahusiano, wadau hao ni katika sekta ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Idara ya Forodha katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  ili kuondoa ucheleweshaji wa meli zinapokuwa katika bandari zetu.

Kuwezesha ongezeko la idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC ambapo idadi ya leseni na vyeti vya usajili ilifikia 1,195 kwa mwaka wa fedha 2021/22 ikilinganishwa na leseni na vyeti vya usajili 941 katika mwaka wa fedha 2018/19 sawa na ongezeko la asilimia 79.

Kuwezesha ongezeko la idadi ya vyeti vya mabaharia waliokidhi masharti kutoka 6,068 katika mwaka 2018/19 hadi kufikia 19,575 katika mwaka 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 31

Kuimarisha udhibiti wa usalama na ulinzi kwenye maeneo ya shughuli za bandari kwa kusimamia urasimishaji wa maeneo 20 ya kibandari katika mwambao wa bahari na maziwa kama Somanga-Lindi,  Kunduchi-Dar es Salaam, Kilongwe-Mafia pamoja na Nyamisati-Pwani.

Kusimamia utekelezaji wa mikataba, itifaki na miongozo inayotolewa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaporidhia. - Mpaka sasa Nchi imeridhia jumla ya mikataba 24 inayojumuisha mikataba mikuu 6 ya lazima.

Kuimarisha usimamizi wa usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira dhidi ya shughuli za meli ili kupunguza matukio ya ajali za vyombo vya majini.

Kaguzi za vyombo vya usafiri majini zilifanyika 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 na kaguzi 4,490 katika kipindi cha  Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023.

TASAC imekuwa likiratibu Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kupambana na Umwagikaji wa Mafuta Baharini.

Kuimarisha Usimamiaji na utoaji wa vyeti vya Mabaharia kwa kuzingatia matakwa ya Shirika la Bahari Duniani (IMO) chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Mafunzo, utoaji vyeti na Ufanyaji kazi kwa Mabaharia.

Kwa mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya vyeti vya Mabaharia 16,718 vilitolewa, Katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka Januari 2023, Shirika liliweza kutoa vyeti 9,570 na takribani vyeti 17,000 vinavyotarajiwa kutolewa ifikapo Juni 2023

Kuongeza mchango katika Mfuko Mkuu wa Serikali mwaka hadi mwaka kutoka Shilingi Bilioni 9.1 katika mwaka wa fedha 2018/19 hadi kufikia Shilingi Bilioni 43.5 katika mwaka wa fedha 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 21 na hivyo kufanya jumla ya mchango wa TASAC katika mfuko mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miaka minne kuwa Shilingi Bilioni  104.5

Kwa sasa Shirika lina ofisi katika maeneo yafuatayo; Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Rukwa, Ukerewe na Geita.

Kukagua meli za nje zinazofika katika bandari zetu kwa mujibu wa Makubaliano ya nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi. 

TASAC tumekagua meli za kigeni 36 kwa kipindi kuanzia julai 2022 hadi desemba 2022, na kuanzia Januari 2023 tumekagua meli za kigeni 37 ambapo tunategemea kukagua meli 61 hadi kufikia juni 2023.

Kuanzisha majadiliano ya kuingia katika makubaliano (Memorandum of Understanding – MoUs) ya kutambuliana vyeti vya mabaharia ili kufungua fursa za ajira kwa mabaharia wetu na nchi 19 ikiwemo Panama, Malta, Cyprus, Qatar, Korea, Ghana pamoja na Jamhuri ya Watu wa China.

FURSA ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA USAFIRI MAJINI

Kuanzisha utaratibu wa kusajili meli kwa masharti nafuu (open registry), kuanzisha maeneo ya ukarabati na ujenzi wa meli katika ukanda wa pwani.

Kuanzisha maegesho ya boti ndogo katika ukanda wa pwani.

Kuanzisha viwanda vya utengenezaji malighafi za ujenzi wa boti za plastiki (fibre) pamoja na kujenga bandari rasmi za uvuvi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo