Dira, Dhamira na Misingi Mikuu
DIRA:
Kuwa Shirika la Uwakala wa Meli linaloongoza katika usimamizi wa usafiri wa majini litakalosaidia kuibadilisha Tanzania kuingia katika mfumo bora wa usafirishaji Duniani.
DHAMIRA:
Kuhakikisha kuwepo kwa huduma za biashara na usafiri wa majini zilizosalama, zakuaminika, zenye uhakika, na mazingira rafiki katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
MISINGI MIKUU:
(i) Uwajibikaji:
Kuwajibika kwa Taifa letu na kwa wadau katika kutekeleza mamlaka na makujumu yaliyo chini ya dhamana ya Shirika;
ii) Uadilifu:
Kuwa mfano wa kuigwa katika mwenendo wetu wa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwenye shughuli zetu zote;
iii) Utaalamu:
Kutumia mkabala unaodhihirisha utaalamu katika weledi, mwenendo, mtazamo na tabia
iv) Haki:
Kutokuwa na upendeleo katika kutekeleza shughuli zetu kwa wateja, watoa huduma na wadau wengine kwa kutoa huduma bila ya upendeleo wala ubaguzi;
v) Uwazi:
Kuwa wazi katika shughuli zetu zote na kuwa tayari kupokea maoni ya wananchi;
vi) Ubunifu:
Tunajitahidi daima kufikia na kutumia teknolojia na njia mpya za ubunifu wa utekelezaji wa mamlaka na dhamana tuliopewa katika kuchangia maendeleo ya Taifa letu.