Majukumu na kazi
Majukumu
na kazi
Kazi na Wajibu wa TASAC vimeelezwa
kwenye Sheria ya Shirika.
WAJIBU:
(a) Kuhimiza usimamizi na shughuli za uwakala
wa meli wenye ufanisi;
(b) Kuhimiza shughuli za bandari na
huduma za meli zenye ufanisi;
(c) Kuhakikisha Usalama na Ulinzi wa
shehena;
(d) Kuhimiza na kutunza mazingira,
usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito;
(e) Kuhimiza ufanisi, uchumi na uaminifu;
(f) Kuendeleza upanuzi wa sekta ya
usafiri kwa njia ya maji;
(g) Kuhimiza ushindani katika biashara ya uwakala
wa meli; na
(h) Kuingia kwenye majukumu ya kimkataba
na watu wengine au kikundi cha watu.
KAZI:
Kwa
mujibu wa kifungu cha 11- 12 cha Sheria ya TASAC Na. 14 ya mwaka 2017,
kazi za Shirika ni:
(1) Kudhibiti
Usimamizi wa Shughuli za
Usafiri kwa
Njia ya Maji, Mazingira, Usalama na
Ulinzi
(a) Kusimamia Sheria ya
meli za Biashara;
(b) Kutimiza
wajibu wa kukagua meli zote za kigeni katika bandari zetu na meli zilizosajiliwa
Tanzania Bara;
(c) Kusimamia
na kuidhinisha vifaa vya huduma za usalama na watoa huduma za usafiri kwa njia
ya maji;
(d) Kusimamia vivuko
e) Kuratibu shughuli za utafutaji na uokozi kwenye bahari, maziwa na mito;
(f) Kusimamia na kuratibu ulinzi na uhifadhi wa mazingira ya bahari, maziwa na mito;
(g) Kutoa taarifa na kujenga uelewa kuhusu mambo yanayohusu mazingira, usalama na ulinzi wa usafiri kwa njia ya maji; na
(h) Kufanya kazi nyingine kama zilivyokasimiwa Shirika kwa mujibu wa Sheria.
(2) Kudhibiti Huduma za
Usafirishaji Majini
(a) Kutoa,
kuongeza muda na kufuta leseni;
(b) Kuweka viwango vya kudhibiti bidhaa
na huduma za kisheria;
(c) Kuweka vigezo na masharti kwa huduma na bidhaa
zinazodhibitiwa;
(d) Kudhibiti viwango vya tozo;
(e) Kufuatilia utendaji wa watoa huduma wanaotambulika kisheria;
(f) Kuwezesha ufumbuzi wa malalamiko na migogoro;
(g) Kufuatilia na kusimamia mwenendo wa kampuni za meli na
watoa huduma wengine wanaotambulika kisheria;
(h) Kufuatilia viwango tozo na malipo ya ziada kwa wanaokiuka ili
uhakikishaji matumizi sahihi katika kipindi cha uhalali wa kutumika;
(i) Kuhimiza, kusajili na kutathmini viwango vya tozo za shehena, sarafu na maghala na
gharama nyingine au kutoza wanaokiuka kuhusiana na huduma za usafirishaji
majini;
(j) Kuzitaka meli zote zinazopakia na kupakua shehena
kwenye bandari za Tanzania Barua
kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa.
ZINGATIA:
Pamoja na kazi zilizoainishwa, TASAC inaweza kufanya kazi nyingine kama Waziri
mwenye dhamana atakavyoipangia.