Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Historia ya Shirika

KARIBU SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA (TASAC)

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tanzania Shipping Agencies Corporation, (TASAC) limeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania Sura ya 415 na kuanza kutekeleza majukumu yake rasmi kuanzia tarehe 23 Februari, 2018 kufuatia Tangazo la Serikali Na. 53 la tarehe 16 Februari, 2018. Majukumu ya Shirika ni kusimamia na kudhibiti sekta ya usafiri wa majini, kuwezesha biashara ya usafirishaji majini na kufanya biashara ya uwakala wa meli.

Misingi Mikuu ya kuanzishwa kwa Shirika ni kuwajibika kwa Taifa na kwa wadau katika kutekeleza mamlaka na makujumu yaliyo chini ya dhamana ya Shirika; Kuwa mfano wa kuigwa katika mwenendo wa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwenye shughuli zote; Kutumia mkabala unaodhihirisha utaalamu katika weledi, mwenendo, mtazamo na tabia; Kutokuwa na upendeleo katika kuhudumia wateja, watoa huduma na wadau wengine kwa kutoa huduma bila ya upendeleo wala ubaguzi; Kuwa wazi katika shughuli zote na kuwa tayari kupokea maoni ya wananchi.

TASAC inatoa huduma kwa weledi na kuhakikisha wateja wanapata huduma iliyo bora na kwa wakati. Huduma zinazotolewa na TASAC ni Biashara ya Usafirishaji, Usalama wa Usafiri wa majini, Usajili wa Vyombo vya Majini na Udhibiti wa Uchumi. Kazi kuu tatu za msingi za Shirika kisheria ni Kuboresha Huduma za Usafirishaji wa Majini; Kuboresha usalama wa usafiri wa Majini, Usalama na Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira ya bahari na Maziwa pamoja na Huduma za biashara za Meli.

Makao makuu ya TASAC yapo Dar es salaam na ofisi nyingine zipo katika mikoa ya Mwanza, Tanga, Kigoma, Rukwa, Mtwara, Geita, Kagera, Mara, Lindi, Mbeya-Kyela na Mwanza-Ukerewe. TASAC pia ina ofisi za Mipakani zipo mikoa ya Kilimanjaro (Holili), Kahama, Tunduma na Sirari (Mara).

Mrejesho, Malalamiko au Wazo