UDHIBITI USALAMA, ULINZI NA UTUNZAJI MAZINGIRA YA USAFIRI MAJINI
UDHIBITI USALAMA, ULINZI NA UTUNZAJI MAZINGIRA YA USAFIRI MAJINI
Imewekwa: 02 February, 2023
UDHIBITI USALAMA, ULINZI NA UTUNZAJI MAZINGIRA YA USAFIRI MAJINI
Usalama, Ulinzi na Utunzaji Mazingira Majini
Kurugenzi ya Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira ya Majini
Kurugenzi hii inadhibiti usafiri kwa njia ya maji kwa kuhakikisha yafuatayo:
- Usalama wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji, wafanyakazi wake, abiria na mizigo;
- Ulinzi wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na miundombinu ya bandari; na
- Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira ya maji kutokana na shughuli zote za vyombo vya usafiri kwa njia ya maji.
- Kurugenzi hii imegawanyika katika sehemu tatu:
- Usajili na Ukaguzi wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji;
- Mafunzo na Utoaji vyeti kwa mabaharia;
- Uongozaji wa vyombo, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira ya usafirishaji kwa njia ya maji.
1.Usajili na Ukaguzi wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji
Kazi za sehemu hii ni kama zifuatazo:
- Kuanzisha mchakato wa kuridhia Mikataba husika ya Kimataifa na utekelezaji wake;
- Kutayarisha Kanuni za Meli zinazoendeshwa kibiashara na kuzipeleka kwa Waziri mwenye dhamana kwa kuidhinishwa;
- Uteuzi wa Wakaguzi wa meli;
- Usajili na Utoaji leseni za meli;
- Ukaguzi na utoaji wa hati za usalama;
- Kupima Ukubwa wa meli;
- Kuweka alama za meli kama vile, mistari ya shehena;
- Shughuli za ukaguzi wa Meli za kigeni zinazotia nanga katika bandari za Tanzania;
- Kudhibiti na kupitisha vifaa vya usalama majini na watoa huduma wake;
- Kudhibiti vivuko.
2. Mafunzo na Utoaji vyeti kwa mabaharia
Kazi za sehemu hii ni kama zifuatazo:
- Kuidhinisha uanzishwaji na mitaala ya vyuo vya mabaharia;
- Kusimamia ajira, ustawi na kushughulikia masuala ya mabaharia;
- Kusimamia sifa na mafunzo kwa mabaharia.
3.Uongozaji wa vyombo Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira ya Usafiri kwa Njia ya Maji
- Kazi za sehemu hii ni kama zifuatazo:
- Kudhibiti ajali za vyombo vya usafiri kwa njia ya maji, uongozaji salama wa meli na uchunguzi wa ajali na matukio yanayopelekea ajali;
- Kusimamia na kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji majini;
- Kusimamia mambo yanayohusu usalama wa bahari, meli, maeneo ya bandari na utekelezaji wa Mkataba wa Usalama wa Meli na maeneo ya Bandari (ISPS Code);
- Kusimamia masuala ya kiusalama bandarini;
- Kudhibiti uchafuzi wa mazingira majini unaosababishwa na vyombo vya usafiri majini;
- Kutoa taarifa kwa wadau na uelewa kuhusu masuala yanayohusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira majini; na
- Kushughulikia mabaki ya meli mbovu na chakavu ikiwemo uondoshwaji wake katika mazingira ya fukwe na maji.