KURUGENZI YA BIASHARA YA HUDUMA ZA MELI
1.0 KURUGENZI YA BIASHARA YA HUDUMA ZA MELI
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kupitia kurugenzi ya Biashara ya huduma za Meli inatekeleza jukumu la Ugomboaji na Uondoshaji wa shehena chini ya sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania kifungu namba 7 Sura 415.
2.0 MAWANDA YA UGOMBOAJI NA UONDOSHAJI WA SHEHENA
TASAC imepewa jukumu la kipekee la Ugomboaji na Uondoshaji wa shehena zinazoingizwa au kutoka nchini kwa bidhaa zifuatazo:
- Silaha na vilipuzi;
- Makinikia;
- Kemikali zinazotumika kwenye kampuni za uchimbaji madini;
- Nyara za Serikali; na
- Wanyama hai kama walivyoainishwa katika Sheria ya Uhifadhi wa wanyama pori.
2.1 MAJUKUMU YA UGOMBOAJI NA UONDOSHAJI WA SHEHENA
Majukumu ya Kitengo cha Ugomboaji na Uondoshaji wa shehena chini ya TASAC yanahusisha:
- Kuhakiki nyaraka za uingizaji na uondoshaji shehena
- Kuratibu ufuatiliaji wa vibali kutoka mamlaka mbalimbali
- Kuandaa kadhia kupitia mifumo ya forodha
- Kufuatilia malipo ya kodi
- Kufuatilia nyaraka za usafiri na usafirishaji kutoka kwa wakala wa meli
- Kushiriki ukaguzi wa shehena kwenye maeneo ya kiforodha
- Kuratibu na kufuatilia ankara za malipo ya gharama za bandari
- Kuratibu usafirishaji wa shehena
- Kutoa ushauri kwa waagizaji na wasafirishaji wa shehena kuhusu taratibu za kiforodha kwa shehena zinazoingia au kutoka nchini.
2.2 MAENEO YA UGOMBOAJI NA UONDOSHAJI WA SHEHENA
Huduma za Ugomboaji na Uondoshaji wa shehena zinafanyika katika maeneo yafuatayo:
- Bandari
- Viwanja vya ndege
- Mipakani na,
Maeneo mengine yaliyoidhinishwa na Mamlaka ya Forodha.
3.0 MAWASILIANO
Wasiliana nasi kupitia anuani na namba za simu zifuatazo;
- Baruapepe;
- Uingizaji wa shehena: importcfa@tasac.go.tz
- Uondoshaji wa shehena: exportcfa@tasac.go.tz.
- Namba ya simu:
+255 222 127 313
+255 222 127 314